Makini Quotes

Quotes tagged as "makini" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwa makini, nadhani, utapata maana ya ujumbe unaopewa na Roho Mtakatifu kwa wale wanaomwamini Mungu au ‘daemon’ (tofauti na ‘demon’) kwa wale wasiomwamini Mungu. Mimi, kwa mfano, huwa najali muda. Jicho langu likicheza au kiungo changu chochote cha mwili kikiuma ghafla na kuacha, au hata kisipoacha, jambo lolote ninalolifikiria muda huo ambapo jicho linacheza au kiungo changu cha mwili kinauma najua ni ujumbe kutoka kwa Mungu na una uhusiano na jambo hilo ninaloliwaza. Hivyo, kuanzia sekunde hiyo napaswa kuwa makini sana na jambo lolote ninalolifikiria.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Siku moja, jambo baya litatokea. Labda babu yako au mnyama wako kipenzi atafariki au shangazi yako atagundulika na kansa. Labda utafukuzwa kazi au utaachika kwa mumeo au mkeo mliyependana sana. Labda rafiki yako kipenzi atapata ajali mbaya ya gari na utatakiwa kupeleka taarifa kwa ndugu na marafiki zake. Kutoa taarifa ya jambo baya kwa mtu ni kazi ngumu sawa na kupokea taarifa ya jambo baya kutoka kwa mtu. Kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya kwa mtu fanya hivyo kwa makini. Toa taarifa ya msiba au ya jambo lolote baya kwa hekima na busara kama Ibrahimu alivyofanya kwa Sara kuhusiana na kafara ya Isaka, si kama Mbenyamini alivyofanya kwa Eli kuhusiana na kutwaliwa kwa sanduku la agano na kuuwawa kwa watoto wake wawili. Jidhibiti kwanza wewe mwenyewe kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya. Angalia kama wewe ni mtu sahihi wa kupeleka taarifa hiyo. Pangilia mawazo ya kile unachotaka kwenda kukisema au unachotaka kwenda kukiandika. Mwangalie machoni, si usoni, yule unayempelekea taarifa kisha mwambie kwa sauti ya upole nini kimetokea.”
Enock Maregesi