Mtoto Quotes

Quotes tagged as "mtoto" Showing 1-10 of 10
Enock Maregesi
“Kitabu cha KOLONIA SANTITA kinaweza kusomwa na watu wenye umri wa kuanzia miaka 13 na kuendelea. Katika umri wa miaka 13 fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali. Watoto katika umri huu wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia, na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na uhakika, kama nadharia ya KOLONIA SANTITA.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwambie mtoto wako maneno mazuri anapokuwa ananyonya na kukuangalia machoni kwa kukukodolea. Maneno utakayomwambia ndiyo yatakayokuwa msingi wa mawazo yake, na ndiyo yatakayoumba maisha yake atakapokuwa mkubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Peter, naomba nitubu kosa. Mimi si mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ni mtoto wa Rais wa Meksiko. Lisa ni mtoto wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” Debbie alisema akitabasamu.
“Hata mimi nilijua ulikuwa ukinidanganya. Lakini mbona Rais wa Meksiko haitwi Patrocinio Abrego?” Murphy aliuliza.
“Utamaduni wa Meksiko ni tofauti kidogo na tamaduni zingine,” Debbie alijibu baada ya kurusha nywele nyuma kuona vizuri. “Hapa, watu wengi hawatumii majina ya pili ya baba zao. Hutumia jina la kwanza la mama la pili la baba; ndiyo maana Wameksiko wengi wana majina matatu. Kwa upande wangu, Patrocinio ni jina la baba yake mama yangu na Abrego ni jina la babu yake mama yangu – kwa sababu za kiusalama.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kilometa mbili na ushei kidogo kutoka katika sanamu la Yesu Mtoto liitwalo Niñopa, katika Kanisa la Parokia ya Manispaa ya Xochimilco ('Sochimiliko') la Iglesia de San Bernardino de Siena, Mexico City, kulikuwa na nyumba ndogo ya siri ('safe house') ya Kolonia Santita iliyojengwa bila uzio wa ukuta au seng’enge isipokuwa miti iliyopandwa kuizunguka bila mpangilio wowote. Ndani ya nyumba hiyo Mpelelezi Maarufu Duniani John Murphy alikuwa akiteswa na magaidi kumi na mbili; waliokuwa wakiendelea kushangaa jinsi alivyookoka katika ajali ya ndege iliyoua watu zaidi ya mia tatu huko Uholanzi, na jinsi alivyoweza kuingia katika ofisi ya siri ya Panthera Tigrisi, kitu kilichomchanganya akili Tigrisi na makompade wote wa Kolonia Santita duniani kote. Bila Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego, na mwanasesere wa nyoka wa Mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Lisa Madrazo Graciano, John Murphy angeanguka.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Bibi Martha Maregesi aliishi maisha mazuri sana hapa duniani. Alibarikiwa na Mungu. Aliishi miaka 84 – siku 30660 badala ya siku 25550 tulizopangiwa na Mungu. Katika uhai wake wote, kwa wale wote aliowalea, hakuna mtoto wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna mjukuu wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna kitukuu chake hata kimoja kilichofariki kabla yake. Bibi yangu ametimiza mwaka mmoja kamili leo hii, tangu amefariki dunia Novemba 4 mwaka 2014 mjini Musoma. Tunamkumbuka leo akiwa amefariki kama tulivyomkumbuka jana akiwa hai. Nguvu ya sala zetu imfanye Mwenyezi Mungu aendelee kumsamehe dhambi zake zote, na amweke mahali anapostahili, Amina.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Jicho ni kiungo cha ajabu zaidi kuliko viungo vyote katika mwili wa mwanadamu baada ya ubongo. Jicho moja linatengenezwa na viungo vidogovidogo zaidi ya milioni mbili, vinavyofanya kazi kwa pamoja bila kukosea. Macho yana nguvu ya ajabu. Huu ni wito kwa akina mama wanaonyonyesha: Usizungumze maneno mabaya mtoto wako mchanga anapokuangalia machoni wakati ananyonya ziwa lako. Neno lolote utakalomwambia, zuri au baya, pamoja na kwamba amekuwa akisikia sauti yako kwa miezi kadhaa akiwa tumboni, litajirekodi katika akili yake isiyotambua bila wewe au yeye mwenyewe kujua. Neno hilo litakuja kumuathiri baadaye atakapokuwa mkubwa. Atakapopevuka, atakapokuwa na uwezo wa kupambanua mambo, atakuwa anaota na kuwaza kile ambacho ulikuwa ukimwambia alipokuwa tumboni; na alipokuwa akinyonya na kukukodolea macho.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mzazi hamjui mtoto wake na mtoto hamjui mzazi wake. Kila mtu hapa duniani ni wa kipekee na wanasayansi wanatuambia kuwa tuko peke yetu hapa ulimwenguni. Lazima tujifunze kupendana na kuheshimiana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usipomlea mtoto wako vizuri, atakapopata shida akiwa mkubwa, na wewe utapata shida pia. Kama unadhani ameshindikana, ongea lugha anayoielewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pombe haina adabu. Ukilewa unakuwa mtoto tena.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiitwa mtoto kidini ina maana una imani na unyenyekevu mbele ya Mungu, kama ambavyo mtoto ana imani na unyenyekevu mbele ya mzazi wake. Lakini ukiitwa mtoto kidunia watu watakudharau.”
Enock Maregesi