Shabaha Quotes

Quotes tagged as "shabaha" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Ndani ya kibweta cha risasi kuna vitu vitano vyenye uwezo wa kulipuka kama vile risasi, kasha, baruti, kitako na fataki. Risasi hutumika kama kombora – kitu kinachoweza kusafiri hewani na kulipuka baada au kabla ya kugonga shabaha – wakati kasha kazi yake ni kuhifadhi vitu vyote vya kibweta kwa pamoja kusudi visisambae. Baruti inayotoa au isiyotoa moshi ni poda yenye uwezo wa kulipuka ambayo ndani yake kuna mkaa, salfa na shura; ambayo husukuma kombora mbele kwa nguvu kubwa baada ya fataki kulipuka kupitia katika kitako cha kibweta. Kitako cha kibweta hutumika kama kiziduo cha risasi kutoka katika chemba ya silaha, wakati fataki kazi yake ni kuwashia baruti.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kasoro za Uzi zilizofanya zisitumiwe tena na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani ni kutokuwa na shabaha imara katika umbali mfupi (hutawanya risasi na huleta madhara makubwa katika umbali mfupi hivyo kuweza kudhuru hata watu wasiokuwa na hatia) na kutokuwa na uwezo wa kutoboa kinga ya risasi dhidi ya magaidi wanaotumia mavazi ya kuzuia risasi, wanaotishia usalama wa rais wa Marekani. Gaidi mwenye mavazi ya kuzuia risasi aliweza kumdhuru rais kwa maana ya USSS kushindwa kumdhibiti. Badala yake, sasa USSS wanatumia FNP90 – zenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi, na ambazo hazileti madhara makubwa katika umbali mfupi na katika umbali mrefu. Bunduki hizi, zenye uwezo wa kubeba risasi 100 katika chemba zake mbili za Kampuni ya Beta ('Century Magazines'), zilitumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume na dhidi ya polisi wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“XM29 OICW ni bunduki iliyowasaidia Vijana wa Tume kubomoa jengo la utawala la Kolonia Santita katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals jijini Mexico City, iliyowasaidia kukamata baadhi ya wakurugenzi wa Kolonia Santita kabla hawajatoroshwa na walinzi wao makomandoo. Bunduki hii inayotumia teknolojia ya OICW ('Objective Individual Combat Weapon') iliyotengenezwa na Kiwanda cha Heckler & Koch cha Ujerumani, ina uwezo wa kufyatua makombora ya HEAB ('High Explosive Air Bursting') yenye ukubwa wa milimeta 20; ambayo hulipuka hewani kabla ya kugonga shabaha, kwa lengo la kusambaza vyuma vya moto katika eneo lote walipojificha maadui. Bunduki hizi hazitumiki tena. Zilitumika mara ya mwisho mwaka 2004.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ndani ya gruneti kuna vitu kumi vyenye uwezo na visivyokuwa na uwezo wa kulipuka kama vile pini, mtaimbo, springi ya mtaimbo, tundu la kuingizia baruti, baruti, fataki, fyuzi, utambi, wenzo na ganda la chuma la pingili kama vipande vya risasi. Pini inapochomolewa, na bomu kurushwa kuelekea kwenye shabaha au kuelekea sehemu nyingine yoyote, wenzo wa usalama huchomoka pia na kuachana na bomu moja kwa moja. Wenzo wa usalama unapochomoka huruhusu mtaimbo ugonge fataki ya kuwashia fyuzi kwa nguvu na kasi kubwa. Fyuzi itawaka kwa sekunde nne kabla ya kuwasha utambi, ambao utawasha baruti ndani ya sekunde moja, kabla ya baruti kulipuka – na kusambaza vipande vya bomu katika kila sehemu ya shabaha.”
Enock Maregesi